Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali ya Mloganzila yafanya upasuaji kupandikiza vifaa vya usikivu

78499 Mloganzilapic

Fri, 4 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji wa kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto waliozaliwa na tatizo la kusikia.

Upasuaji huo umefanywa kwa watoto watatu akiwemo mmoja kutoka nchini Rwanda aliyepandikizwa katika masikio yote mawili.

Mloganzila inakuwa Hospitali ya pili ya umma kuanza kutoa matibabu hayo yaliyoanza kutolewa mwaka 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Akizungumza leo Ijumaa Oktoba 4, 2019 kaimu naibu mkurugenzi wa Hospitali ya Mloganzila,  Dk Julieth Magandi amesema kufanikiwa  kwa upasuaji huo ni mafanikio makubwa kwa taasisi hiyo iliyoanza kutoa huduma miaka michache iliyopita.

Dk Magandi amesema kufanikiwa kwa upasuaji huo wa kibingwa imedhihirisha kuwa Tanzania sasa imebobeba katika matibabu na imeanza kuaminika kwa kuwapata wagonjwa kutoka nje ya nchi.

“Uwezo wa wataalam wazalendo katika kufanya upasuaji huu umefikia asilimia 90 wakati kwenye kuwasha vile vifaa vya usikivu imefikia asilimia 100.”

Pia Soma

Advertisement
“Upasuaji huo kufanyika nchini pia unasaidia kupunguza gharama kwa sikio moja hugharimu  Sh36 milioni tofauti na nje ya nchi ambapo hugharimu kati ya Sh80 milioni hadi Sh100 milioni,” amesema Dk Magandi.

Chanzo: mwananchi.co.tz