Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali ya Hydom Manyara yanunua mashine za X-ray

65180 Pic+haidom

Tue, 2 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbulu. Hospitali ya Rufaa ya Haydom wilayani Mbulu, mkoani Manyara Tanzania, imenunua mashine mpya ya kisasa ya uchunguzi (X-ray) kwa lengo la kuhudumia wagonjwa wengi, kuongeza ufanisi na kutoa huduma kwa urahisi zaidi.

Mkurugenzi wa hospitali ya Haydom, Dk Emmanuel Nuwass  akizungumza jana Jumatatu Julai 1, 2019 alisema mashine hiyo ya kidijitali imenunuliwa kwa gharama ya Sh300 milioni.

Dk Nuwass alisema mashine hiyo ya kisasa kutoka Ufaransa itasababisha ufanisi mkubwa katika utendaji kazi wake katika kuwahudumia wagonjwa wa hospitali hiyo tofauti na awali.

Alisema mashine hiyo ina uwezo mkubwa wa kupiga picha kwa ubora na muda mfupi tofauti na ile iliyokuwa inatumika kwa teknolojia ambayo imepitwa na wakati.

"Mashine hii ni ya kisasa na ya kipekee kwani kwa hapa nchini zipo mbili za toleo hili katika hospitali ya Haydom na hospitali ya Bugando jijini Mwanza," alisema Dk Nuwass.

Mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo, John Matle aliyekuwa hospitalini hapo amepongeza jitihada za Dk Nuwass katika kuboresha miundombinu ya hospitali ya Haydom.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz