Dar es Salaam. Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam imesema kambi ya kutoa huduma ya upasuaji wa kubadili na kuboresha maumbile au ngozi iliyokakamaa kwa wanawake na watoto wa kike masikini itafanyika mara mbili mwaka 2019 badala ya mara moja kama iliyokuwa miaka minne iliyopita tangu kuanzishwa kwake.
Kambi hiyo inalenga kuwasaidia wanawake na watoto wa kike maskini wenye ulemavu uliosababishwa na ukatili wa nyumbani, kuungua na ajali na matibabu yake yanatolewa bure.
Akizungumza na wanahabari leo Jumatatu, Juni 10, 2019 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Aga Khan, Dk Aidan Njau amesema awamu ya kwanza itaanza mwezi huu na inayofuata itafanyika Agosti.
"Kumekuwa na mwitikio mkubwa katika kambi hii na matunda yake yameonekana ndio maana tumeamua tufanye mara mbili kwa mwaka huu ili kuwapa fursa ya kupata huduma za matibabu haya. katika awamu zote mbili tunatarajia kuwafikia wanawake na watoto kike takriban 100,” amesema Dk Njau
"Shughuli hii tutaifanya tukishirikiana na madaktari bingwa kutoka Muhimbili (Hospitali ya Taifa), Marekani na Aga Khan. Ushirikiano huu unalenga kuimarisha utaalamu wa upasuaji kwa ajili ya kushughulikia hitiji la tiba ya upasuaji wa kubadili na kuboresga maumbile," amesema
Dk Njau amefafanua kambi kubwa ya uchunguzi wa kuwatambua wagonjwa wengine uhitaji wa matibabu hayo utafanyika katika Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam na vituo vyake vya afya vilivyopo mikoa ya Mwanza, Mbeya, Dodoma, Tabora, Bukoba, Tanga, Iringa na Morogoro, kuanzia Juni 15.
Pia Soma
- Ofisa wa TRA na askari polisi, kortin kwa kuomba rushwa ya Sh2 milioni
- LIVE: MAGUFULI AKIWAAPISHA VIONGOZI NA KUPOKEA GAWIO KUTOKA KAMPUNI YA BHARTI AIRTEL IKULU DAR
- Muswada kila bodaboda kuwa na bima ya afya wanukia
"Upasuaji huu ni gharama sana kwa mtu mmoja anaweza akalipia Sh 5milioni kwa ule upasuaji mkubwa wakati mdogo analipia Sh 2milioni, lakini kupitia kambi hii tunatoa bure huduma tukishirikiana na wadau mbalimbali," amesema Dk Al.