Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali sita zapatiwa mashuka 1,050

Pic Mashuka Hospitali sita zapatiwa mashuka 1,050

Wed, 11 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu ametoa wito kwa kampuni,taasisi, mashirika na jamii kushirikiana na Serikali kuboresha maeneo ya kutolea huduma za afya ili kusaidia upatikanaji wa huduma bora.

Dkt. Jingu amesema hayo leo Septemba 10, 2024 wakati akipokea shuka zenye thamani ya shilingi Milioni 25 kwa ajili ya hospitali sita za rufaa za mikoa ambazo zimetolewa na Chama cha Ushirika cha TANESCO kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, Temeke, Ilala, Amana, Njombe, Katavi na Simiyu.

Dkt. Jingu amesema msaada huo ni kiashirio cha kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha vitendea kazi kwenye hospitali mbalimbali nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live