Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali rufaa Iringa kutoa viungo bandia

Iringaapic Data Hospitali rufaa Iringa kutoa viungo bandia

Sun, 12 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Iringa imeanza kutoa huduma za viungo bandia kwa wagonjwa waliopoteza baadhi ya viungo ajalini jambo linalotajwa kuwa litapunguza gharama kwa wagonjwa waliokuwa wakisafiri mikoa jirani kusaka huduma hiyo.

Hayo yanabainishwa na kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Iddy Omary katika uzinduzi wa jengo la maabara ya vifaa tiba saidizi.

"Hizi huduma za viungo bandia saidizi zilikuwa zinaendelea, ilikuwa ngumu kumuelekeza mgonjwa kuwa mguu wake unatakiwa kukatwa na kuanza maisha mapya bila mguu mmoja ukizingatia huduma hizi zilikiwa zinapatikana Mbeya, Muhimbili, KCMC na gharama zake zilikuwa kubwa.”

“Unapoanza kumuandaa mgonjwa na kufika katika kipengele cha gharama wakati mwingine mgonjwa alikuwa anapata matatizo ya afya ya akili kutokana na ukubwa wa gharama. Kwa sasa tunakushukuru mdau wetu Asas kwa jengo hili  na vichenza kwa kutusaidia upatikanaji wa vifaa tiba kwani kwa sasa huduma hii itapatikana katika hospitali yetu na kwa bei nafuu,” amesema.

Awali akizindua  jengo hilo mdau wa sekta ya afya ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Asas Group,  Salimu Abri amesema kwa sasa mahitaji ya viungo bandia yamekuwa mengi kutokana na ajali nyingi za bodaboda.

"Watu wengi walikuwa wanakwenda hospitali nyingine kupata huduma ya viungo bandia lakini kwa sasa huduma hii inapatikana hapa tena kwa gharama nafuu,  pia vijana wa bodaboda waendelee kuchukua tahadhali kuepuka ajali," amesema Salim.

Advertisement

Chanzo: www.mwananchi.co.tz