Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali 95 zafungiwa Tanzania tangu mwaka 2018

89602 Hospital+pic Hospitali 95 zafungiwa Tanzania tangu mwaka 2018

Mon, 23 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania imezifungia hospitali 95 kuanzia Julai 2018 hadi Juni 2019 kutokana na kukosa sifa.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa tume hiyo, Profesa Lazaro Busagala wakati akifunga mafunzo ya udhibiti na usalama wa mionzi katika idara ya radiolojia nchini.

Mafunzo hayo yaliwahusisha watumishi 104 wanaofanya kazi katika idara ya afya kutoka mikoa yote nchini,  kujifunza namna ya udhibiti na usalama wa mionzi katika maeneo yao ya kazi.

Profesa Busagala amesema mwaka 2018 walikagua Hospitali 664, kati ya hizo 105 zilifungiwa, “kati ya zilizofungiwa 10 zilikidhi vigezo na kufunguliwa na kubaki 95 ambazo hazijafunguliwa.”

Amesema mwaka 2019 wameshaanza ukaguzi wa hospitali mbalimbali na kwamba tatu tayari zimefungiwa.

Amesema lengo ni kuhakikisha mtu yeyote anayetumia mionzi kuwa na utaalamu wa kutosha kuhusu matumizi  na namna ya kutumia mionzi hiyo ili isiweze kuumiza wengine ama kuleta madhara kwa jamii husika.

Kaimu Mkurugenzi wa teknolojia na ufundi wa TAEC, ,Firmi Banzi amesema  lengo la kutoa mafunzo hayo  kila  mwaka ni kuhakikisha watumiaji wa  mionzi wanakuwa na uelewa wa  kutosha kuhusu matumizi sahihi ya mionzi kwa faida ya jamii.

Chanzo: mwananchi.co.tz