Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali 11 kuto tiba kwa njia ya mtandao

Watoto 22 Wafanyiwa Upasuaji Wa Moyo Ndani Ya Siku 6 Hospitali 11 kuto tiba kwa njia ya mtandao

Tue, 14 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umeunganisha hospitali 11 na mawasiliano ya kidijiti kuziwezesha kutoa huduma ya tiba kwa mtandao.

Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba alisema hayo jijini Dodoma na akasema mfuko huo unatekeleza kwa kushirikiana na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).

Mashiba alisema pia huduma hiyo inaunganishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) na hospitali za rufaa za mikoa ikiwamo ya Morogoro ambayo tayari imeunganishwa. Alisema kazi inaendelea kuunganisha huduma hiyo katika hospitali za Ruvuma, Tanga, Katavi, Nzega na Chato.

Mashiba alisema kwa upande wa Zanzibar wanaunganisha huduma hiyo katika hospitali za Abdalla Mzee na Mnazi Mmoja. Mashiba alisema kwa upande wa Zanzibar, UCSAF imejenga vituo 11 vya tehama ambavyo vinasaidia kutoa mafunzo na akasema vinne vimejengwa Pemba na saba Unguja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live