Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Homa ya nyani haipo Tanzania

Monkey Pox Homa ya nyani haipo Tanzania

Tue, 24 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Afya Tanzania imesema hayupo wala hajawahi kuwepo Mgonjwa wa homa ya nyani Nchini Tanzania (Monkeypox) lakini hata hivyo imetaka Watu wote kuendelea kuchukua hatua za kujikinga na kuzuia magonjwa ya kuambukizwa na yale ya mlipuko ikiwa ni pamoja na usafi binafsi na wa mazingira.

Katika taarifa yake, Wizara ya Afya imewataka pia Wananchi kutogusa au kula mnyama anaeumwa au mzoga na vilevile kutogusa vitu vilivyotumika na mnyama mgonjwa au mzoga.

“May 16, 2022, Shirika la Afya Duniani lilitoa taarifa ya kuwepo kwa mlipuko kwa Monkeypox nchini Uingereza na mpaka kufikia May 20, 2022 Watu 38 duniani walithibitika kuwa na ugonjwa huo ambapo Uingereza walikua 9, Ubelgiji (2), Ufaransa (1), Italia (1), Ureno (14), Hispania (7), Uswisi (1), Canada (2) na Marekani (1), kati ya wagonjwa hao 38, wawili (2) lakini hakukuwa na kifo chochote.

“Monkeypox ni ugonjwa unaotokea mara nyingi kwenye nchi za Afrika ya kati na Afrika ya Magharibi kweye misitu ya mvua za kitropiki ambapo wanyama kama nyani, panya na kindi wenye virusi hivyo ndipo wanapoishi ambapo Binadamu anaambukizwa baada ya kugusa mnyama mwenye maambukizi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live