Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Homa ya dengue yaua 13

68479 Dengue+pic

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania  imesema homa ya dengue imeua watu 13 nchini huku 6,677 wakiugua ugonjwa huo.

Takwimu hizo zimetolewa leo Jumamosi Julai 27, 2019 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika uzinduzi wa mkakati wa Taifa wa kupambana na mbu na wadudu wengineo katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Waziri huyo amesema awali takwimu zilionyesha vifo sita  lakini Serikali ilifanya tathmini upya na kupata takwimu sahihi.

"Tulikuwa na takwimu za vifo sita lakini Serikali tumefanya tathmini upya na kupata idadi ya vifo 13 nchi nzima na Mkoa wa Dar es Salaam ndiyo unaongoza kwani umekuwa na wagonjwa 6,631 na vifo 11," amesema.

Amesema ugonjwa huo kwa sasa unapungua kwa maelezo kuwa Juni, 2019 kulikuwa na wagonjwa 536 na tangu kuanzia Julai hadi leo kuna wagonjwa sita pekee.

"Homa ya dengue ilipoingia watu wakapata taharuki kubwa , mikakati mipana ya kupambana na dengue ikapangwa, lakini ikaonekana bado kuna tatizo kwa kuwa takwimu za Malaria nchini zinaonyesha watu milioni  5.6 milioni wanaugua kila mwaka na vifo 4,390.”

Pia Soma

“Tumekuja na mkakati mpana zaidi kupambana na wadudu wadhurifu, wakiwemo mbu, viroboto, chawa, mende, Ndorobo, konokono, kunguni, nzi na papasi," amesema Waziri Ummy.

Chanzo: mwananchi.co.tz