Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi ndio faida 10 za kula tikiti maji

73969 Tikiti+pic

Tue, 3 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Matunda ni kati ya chakula muhimu katika mwili mwanadamu.

Wataalamu wa afya wanasema tunda hilo ni chanzo kikuu cha protini, mafuta, nyuzinyuzi, wanga, calcium, phosphorus, chuma, vitamin A,B6, C na Potasium na virutubisho vingine vingi.

Mtaalamu wa Lishe kutoka Jukwaa la Lishe Tanzania (Panita) Deborah Essau amesema tikiti maji linasaidia kuimarisha misuli na mfumo wa fahamu na kuusaidia ufanye kazi zake vizuri.

Essau amesema kama mfumo wa fahamu utafanya kazi ipasavyo basi tunda hilo linaweza kukuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu.

Mtaalamu mwingine, Matrida Erick kutoka Shirika la Furaha Pamoja Foundation amesema asilimia 92 ya tunda hilo ni maji, lina vitamini A ambayo huboresha afya ya macho na vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili.

Deborah amsema vitamini hiyo pia huponya majeraha, hukinga uharibifu wa seli na kuboresha afya ya meno na fizi.

Pia Soma

Advertisement   ?
Ameeleza tunda hilo lina vitamini B6 ambayo husaidia ubongo kufanya kazi vema, kubadilisha protini kuwa nishati na ni chanzo cha madini ya potasiamu.

Wataalamu wa lishe pia wanahamasisha ulaji wa tikiti maji kwa madai kuwa huongeza nguvu za kiume hasa pale mtu anapokula pamoja na mbegu zake.

Wanashauri tunda hilo kuliwa walau mara mbili kwa wiki.

Chanzo: mwananchi.co.tz