Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi hapa sababu za watu kupofuka, kuona kwa shida

05aacd2b340e1f664d1914439c4e61bf.jpeg Hizi hapa sababu za watu kupofuka, kuona kwa shida

Sat, 16 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TAKRIBANI asilimia moja ya Watanzania wana upofu na asilimia tatu wana uoni hafifu wa hali ya juu, imefahakika huku sababu za hali hiyo zikitajawa.

Mkuu wa Idara ya Macho katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Dk Evarista Mgaya alitoa takwimu hizo juzi katika maadhimisho ya siku ya macho duniani.

“Magonjwa yanayosababisha kutokuona ni pamoja na mtoto wa jicho ambao huweka ukungu kwenye kioo cha jicho. Hali hii inachangia zaidi ya asilimia 50 ya kutoona. Mwaka jana kati ya pasuaji 1,000 zilizofanyika, zaidi ya 700 ilikuwa mtoto wa jicho,” alisema.

Aliendelea kueleza kuwa visabishi vingine vya upofu na uoni hafifu ni makovu kwenye jicho yanayochangia zaidi ya asilimia 20 ya ulemavu.

Aliishukuru serikali kuimarisha mpango wa chanjo za surua na vitamin A, hatua ambayo imechangia kiasi kikubwa kupunguza matatizo ya macho.

Kwa mujibu wa Dk Mgaya, watu wengine wanapata makovu kwenye macho kutokana na shughuli za kiuchumi kama kuponda mawe, kuchomelea vyuma au watoto kuumizana kwa vijiti katika michezo yao.

Ilielezwa kwamba shinikizo (presha) la jicho linachangia asilimia 10 ya upofu duniani na mtu yeyote anaweza kupata ispokua zaidi ni kwa wale wenye umri zaidi ya miaka 40, wanaorithi na wenye ugonjwa wa kisukari.

“Tunawashauri wananchi kufuata maelekezo ya wataalamu kulingana na tatizo lilivyo, kama vile kuvaa miwani, kutonunua dawa bila ushauri wa daktari, kula mlo kamili na kufanya mazoezi bila kusahau kupima afya ya macho walau mara moja kwa mwaka hata kama mtu hana shida yeyote,” alishauri.

Chanzo: www.habarileo.co.tz