Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi hapa sababu wajawazito kujifungua kabla ya muda

Njiti Watoto Hizi hapa sababu wajawazito kujifungua kabla ya muda

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daktari bingwa wa magojwa ya Wanawake na uzazi kwa kina Mama katika hospitali ya Taifa Muhimbili upande wa Mloganzila Dkt. Hilary Kizwi amesema katika kipindi cha wiki 37 za ujauzito kimegawanyika katika miezi mitatu ambapo Mtoto akizaliwa kabla au baada ya wiki 28 anaweza akawa njiti kutokana na kutokamilika.

Amesema hayo katika kipindi cha Mirindimo ya Asubuhi cha TBC Taifa ambacho kimekita kambi hospitalini hapo.

Dkt. Kizwi ameeleza sababu za kujifungua kabla ya siku kukamilika ni pamoja na Mjamzito kupata uchungu kabla ya muda na pili ni matatizo ya kitabibu.

Ameeleza kuwa vyanzo vingine ni maambukizi katika njia ya mkojo na uzazi, kupasuka chupa ya maji kutokana na maambukizi na ujauzito wa zaidi ya mtoto mmoja.

Dkt. Kizwi ameshauri ni vema Mama anapogundua hali hiyo akae chini ya uangalizi ili kuepusha ongezeko kubwa la msukumo katika mfuko wa uzazi.

Pia, ameeleza umuhimu wa Baba na Mama kuhudhuria kliniki pamoja kwa kuwa kunasaidia mama kuwa na utulivu wa hisia na akili kipindi cha ujauzito.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live