Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haya ndiyo makundi hatarishi ya TB inayoua watu 70 kila siku duniani

Tuberculosis X Ray 1gg Haya ndiyo makundi hatarishi ya TB inayoua 70 kila siku duniani

Thu, 30 Sep 2021 Chanzo: IPPmedia

Ripoti ya Shirika la Afya Duniani WHO inaonesha kuwa Tanzania inaendelea kupiga hatua katika kupunguza kasi ya maambulkizi ya ugonjwa Kifua Kikuu kwa asilimia 18 kwa mwaka 2020.

WHO lilitathmini nchini, kwa kushirikiana na wataalamu kutoka nje na ndani, kuona namna tulivyofikia malengo tuliyojiwekea kwenye mpango mkakati wa mwaka 2015, ikiwamo kuongeza kasi ya kuwafikia wagonjwa kwa asilimia 29 zaidi.

Ripoti hiyo iliyotolewa mwaka jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Zainab Chaula, katika kilele cha mkutano wa kupokea taarifa ya tathmini ya mpango mkakati wa tano wa mwaka (2015-2020) wa Kifua Kikuu na Ukoma.

Ni hatua nzuri zilizofikiwa, lakini itapendeza iwapo mapambano hayo yatapanuliwa kwa kumshirikisha kila mtu, huku elimu kwa umma ya kutambua dalili za TB ikipewa kipaumbele zaidi.

Kwa nini? Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa ugonjwa huo unaua watu 74 kila siku, huku makundi hatarishi yakitajwa ni ya wanaotumia dawa za kulevya, wakiwamo wanaojidunga sindano.

Dk. Saitole Laizer, anatoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali, katika uzinduzi wa muungano wa wadau wa kupambana na kifua kikuu nchini, kwamba ugonjwa huo bado ni tishio, ingawa wengi hawajui kuwa unaua. Kimsingi, utaendelea kuua ikiwa juhudi za makusudi hazitachukuliwa haraka.

Anafafanua kwamba, katika takwimu hizo za mwaka 2018, vipimo vinaonyesha kati ya watu 133,000 wanaopimwa, 227 hukutwa na maambukizi, hivyo kuifanya Tanzania kuwa na wagonjwa 1,600 wa TB sugu, na kati yao 400 waligundulika mwaka jana pekee.

Kuisaidia katika vita hiyo, waliowahi kuugua wakatibiwa na kupona, wanaweza kuwa walimu wazuri kwa umma kuzijua dalili za TB, ili waende kupata vipimo sahihi, badala ya kuamini wamelogwa.

Watu hao watakapotumika vizuri kutoa elimu, watasaidia kuwafanya Watanzania watambue jinsi ugonjwa huo unavyoenezwa na watakuwa makini kuepuka mazingira hatarishi yanayoweza kusababisha wakaambukizwa.

Hao wanajua kuwa kuboresha usafi wa mazingira, kuishi katika nyumba zenye hewa safi na kuepuka msongamano wa watu, ni mojawapo ya njia ya kuepuka TB inayotajwa inatibika licha ya kuwa hatari, inatibika.

Pia, wanajua kwamba kupungua uzito, kutokwa na jasho jingi nyakati za usiku, kukohoa kwa muda wa wiki mbili mfululizo, ni dalili nyingine za mtu kuwa na ugonjwa huo, hivyo si vibaya wakatumika kuelimisha.

Kwa kutambua mazingira hayo hatarishi, ni wazi kila Mtanzania atajihadhari na kuchukua hatua anapohisi dalili, kutokana na ugonjwa huo unaweza kumpata yeyote na kwa wakati wowote.

Hivyo, suala la elimu kwa umma likiwekewa mkazo, wale ambao wamekuwa wakiugua na kukimbilia kwa waganga wa kienyeji, nao watambue umuhimu wa njia sahihi za matibabu.

Ni namna bora inayomfanya kila mtu atambue ni elimu kwa umma, hasa kwenye maeneo ambako nyumba zimesongamana, ni mazingira yanayoweza kusababisha wakazi wa huko kupata ugonjwa huo kirahisi.

Ushauri wa kushirikisha kundi hilo katika utoaji wa elimu ninautoa, kwani siamini kama watumishi wa sekta ya afya pekee yao wanaweza kutosha kuzunguka nchi nzima kuelimisha umma, hivyo wakiongezewa na hao niliowataja, inawezekana kukawa na matokeo chanya zaidi katika kukabiliana na TB.

Ikumbukwe, wataalamu wa afya wanaitaja TB katika orodha ya magonjwa duniani, unaua watu wengi kuliko katika idadi ya juu kutoka orodha ya magonjwa hatari, inaambukiza kwa kasi, lakini inatibika.

Sababu za kifua kikuu kuua kwa kasi, zitajwa kuwa zinachangia ugonjwa huo kuua, ni watu wanaoumwa kukatisha kutumia dawa kabla ya muda waliopangiwa na hivyo kujikuta wanapoteza maisha.

Nionavyo, elimu ikitolewa inaweza kusaidia kuwafanya watu kumaliza dozi, badala ya kuishia njiani na kujisababishia athari mbaya, ambazo huenda wangeziepuka kama wangetimiza masharti ya wataalamu wa afya.

Chanzo: IPPmedia