Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haya hapa madhara ya kutumia simu bila kunawa

B855247054ed1c2298e108c2dff98a13 Haya hapa madhara ya kutumia simu bila kunawa

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SIMU za mkononi zimetajwa kuwa ni hatari katika kuhifadhi na kusambaza vijidudu vya magonjwa ya kuambukiza kama zitashikwa bila kunawa mikono wakati au baada ya kutoa huduma.

Hayo yalisemwa jijini hapa mwishoni mwa wiki na Mfamasia, Erick Venant alipokuwa akitoa mada ya uelewa na umuhimu wa unawaji mikono kwa watumishi wa afya

kwenye Kongamano la Afya Tanzania (THS) ikiwa ni miongoni mwa mada saba zilizotolewa na Mradi wa HPSS-Tuimarishe Afya unaotekelezwa na Shirika la Swiss TPH kwa ufadhili wa Shirika la Ushirikiano na Maendeleo la Uswizi (SDC).

Alisema walifanya utafiti uliolenga kutathmini maarifa, uwepo na upatikanaji wa vifaa vya usafi wa mikono na uzingatiaji wa mwongozo wa usafi wa mikono wa Shirika la Afya Duniani (WHO), ambapo ulionesha zaidi ya asilimia 75 ya watumishi wa afya mkoa wa Dodoma wamepata mafunzo ya usafi wa mikono na kuwa na uwezo wa kufikia vifaa vya kunawa mikono.

Aidha, alisema asilimia 63 ya madaktari, wauguzi na wanafunzi walio kwenye mafunzo kazini, 270 waliofanyiwa utafiti kwenye mkoa huo walibainika wana uelewa kuhusu unawaji mikono kulingana na mwongozo wa WHO, huku asilimia 2.6 wamekuwa wakitekeleza kikamilifu mwongozo huo.

Pia alisema kwenye utafiti huo walibaini asilimia 34 ya simu za watumishi zilizotumika kama sampuli kwenye utafiti huo zilikuwa zina bakteria mbalimbali kama staphylococci ambao wana usugu kwa dawa ya penicillin na upinzani wa tiba kwa dawa aina ya Erythromycin, Clindamycin na Gentamycin.

Chanzo: www.habarileo.co.tz