Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatima ya matibabu binti wa kidonda Jumanne

53352 Pic+kidonda

Tue, 23 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hatima ya matibabu ya Mariam Rajab mwenye kidonda mgongoni itajulikana Jumanne ijayo baada ya madaktari kukamilisha uchunguzi na majibu ya vipimo alivyofanyiwa kutolewa.

Majibu hayo ndiyo yatakayoeleza ni aina gani ya kidonda kinachomsumbua binti huyo ili matibabu yake yaanze kufanyika kwa haraka.

Akizungumza na Mwananchi juzi, mkuu wa kitengo cha mawasilianoHospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha alisema baada ya vipimo kufanyika kinachosubiriwa ni majibu ambayo yatakuwa tayari Jumanne.

“Hadi Jumanne majibu yote yatakuwa tayari na tutawaeleza hatua itakayoendelea ila kwa sasa anaendelea kuangaliwa kwa ukaribu na madaktari na afya yake iko vizuri,” alisema.

Taarifa za ugonjwa wa Mariam zilisambaa siku chache zilizopita kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha binti huyo akiomba msaada wa matibabu kutokana na kidonda hicho cha muda mrefu.

Mkuu wa idara ya upasuaji MNH, Dk Ibrahim Mkoma amesema matokeo ya vipimo vilivyochukuliwa ndiyo yatakayotoa mwongozo ni aina gani ya matibabu ambayo Mariam anatakiwa kupatiwa huku akieleza kuwa mara nyingi vidonda vya aina hiyo vina uhusiano na saratani.



Chanzo: mwananchi.co.tz