Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatari upasuaji kubadili maumbile!

Maumbile Maumbileeee Hatari upasuaji kubadili maumbile!

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

"Wanawake kwa ujumla huwa hawapendi kuchumbiwa na wanaume wafupi zaidi yao. Ugumu unakuja pale wakati mwingine unapopata hisia kwamba sitampata mke."

Kauli hii inatoka kwa Sam, mwanaume Muingereza mwenye umri wa miaka 30-ambaye ni sehemu ya mtindo wa upasuaji wa kubadilisha muonekano miongoni mwa wanaume unaoshamiri katika mataifa ya Marekani, uingereza na hata Uhispania wa kurefusha miguu ili kuongeza kimo cha urefu wa mwili

Upasuaji huu unahusisha kupasua mifupo ya miguu ili kuongeza sentimita chache.

Sam anasema anashukuru upasuaji wake, kwani umemuwezesha kukuongeza sentimita 8 za urefu kutoka mita 1.62 hadi mita 1.70 katika kipindi cha miezi michache

"Nimekuwa kila mara nikipigania kuwa mrefu na kupata mafanikio yanayohusiana na urefu. Hiyo ndio maana ilibidi nitafute suluhu langu mwenyewe ," Tom Brada alimwambia mwandishi wa BBC.

Upasuaji huu unahusisha kipindi cha wiki kadhaa za uponaji na mchakato wa uponaji ambapo mgonjwa hawezi hata kutembea kwa miezi kadhaa.

Lakini sio hilo tu, kwa visa fulani wanaume hulipa karibu dola za Kimarekani US$70,000 kupata inchi chache za kuongeza kimo cha urefu wao.

"Ni upasuaji unaoumiza sana, unaojumuisha mchakato mrefu wa kupona kwasababu sehemu ya mfupa laini inaongezewa, kwahiyo huwezi kutembea hadi mfupa ule uweze kuhimili uzito wam wili tena ," aliiambia BBC, daktari wa upasuaji Kevin Debiparshad, ambaye hufanya upasuaji huu.

Debiparshad amewafanyia upasuaji wa aina hii hadi watu 50 katika Las Vegas kwenye taasisi ya LimbplastX , ambako anasema ameshuhudia kuongezeka kwa idadi ya wanaume wanaotaka kuongeza kimo cha mwili wao kwa njia ya upasuaji huu.

Ukarabati, na sio kwa ajili ya utanashati

Upasuaji umezingirwa na utata

Kwa pamoja Chama cha madaktari wa upasuaji wa kubadilisha maumbile na Chama cha Maraktadi wa mifupa nchini Marekani wameielezea BBC kwamba upasuaji wa kurefusha miguu ni mchakato wa upasuaji wa mifupa kwa lengo la kubadilisha muonekano wa mtu.

Muasisi wa mbinu hii alikuwa ni daktari wa mifupa ambaye alivumbua tiba ya ukarabati wa mifupa kwa ajili ya wanajeshi waliokatika viungo vyao wakati wa Vita Kuu ya II ya Dunia.

Jina lake alikuwa ni Gavril Ilizarov, daktari aliyeheshimiwa ambaye wakati ule kwa kuarifiwa , pamoja na majaribio aliyokuwa nayo aliyoyafanya wakati alikuwa mwanafunzi, kwamba mfupa wa mguu , ulikuwa na uwezo wa kurefushwa na "kujaza" pengo ambalo lilibakia katikati ya sehemu mbili wakati eneo lililovunjika linapojazwa.

Kulingana na maelezo ya madaktari kadhaa wa upasuaji waliozungumza na BBC, tiba ya kawaida ni kiama ifuatavyo : fkwanza, shimo linachimbwa na na kutengenezwa katika mifupa wa miguu, ambayo inagawanywa mara mbili.

Halafu chuma huwekwa ndani ya mfupa na kushikiliwa kwa skrubu.

Chuma hicho hukazwa zaidi taratibu kwa takriban milimita 1 kila siku, kinavutwa hadi kiwango cha urefu anachotaka mgonjwa kitakapofikiwa na baadaye mifupa yake inaachwa kuendelea kupona tena.

Kulingana na Sam na wagonjwa wengine, matibabu hayo sio ya maumivu tu, bali uponaji wake unaweza kuwa ni wa muda mrefu sana

Hatari

Haya ni mojawapo ya mambo yanayoangaliwa na madaktari wakati wanapotazama : hatari zinazohusika katika kufanya upasuaji huu kwa lengo la kubadili muonekano.

Baadhi ya wataalamu wanaonya juu ya uwezekano wa mgonjwa kupata matatizo, ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa mishipa kiasi kwamba unatokea uwezekano wa mifupa kushindwa kufanya kazi tena.

Lakini sio suala la mwili tu : wataalamu wanaonya juu ya hatari za kisaikolojia ambazo zinapaswa kutiliwa maanani, kwani ukweli ni kwamba baadhi ya wagonjwa hawa wanaweza hali ya - body dysmorphia- ambapo mtu hukasirishwa na muonekano wa mwili wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live