Kwa mujibu wa Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2015/16, idadi ya wanaojifungulia vituo vya afya na kwa msaada wa watu wenye ujuzi inazidi kuongezeka Tanzania mwaka hadi mwaka.
Ripoti ya utafiti huo iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar (OCGS) inaonyesha kuwa mwaka 2015/16 asilimia 63 ya watoto walizaliwa kwenye vituo vya afya ikiwa ni ongezeko kutoka asilimia 50 au nusu ya watoto waliofanyiwa utafiti mwaka 2010.
Licha ya ongezeko hilo, changamoto inabaki kwa wajawazito wanaoishi vijijini ambao hulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwa sababu ya zahanati kuwa mbali na maeneo wanayoishi.
Hali hiyo inaweza kuhatarisha afya zao na watoto.