Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna utafiti unaonesha chanjo ya Covid-19 ina madhara-Dk Janabi

862c56c1b52500469543b5bfc897b01d Hakuna utafiti unaonesha chanjo ya Covid-19 ina madhara - Dk Janabi

Sun, 15 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKURUGEZI wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi amewataka watu kuacha kutabiria chanjo ya Covid -19 kuwa ina madhara wakati hakuna utafiti uliofanyika kubaini hilo.

Prof Janabi aliyasema hayo Juzi wakati akihojiwa na kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) alisema hakuna madai ya kweli kuwa chanjo hizo zinasababisha matatizo ya uzazi au kugandisha damu.

“Najiuliza swali kubwa, hizi chanjo zimeanza kutolewa mwanzoni mwaka huu kwa sababu leseni zimetolewa Desemba 31 mwaka jana kwa chanjo zote hivyo sasa ni miezi saba tangu zianze kutolewa. Kwa hiyo hilo la uzazi linapozungumziwa, hawa watu wameshika ujauzito lini? Hata ingekuwa Januari bado hawajajifungua kwa hiyo ni sawa na kusema ngoja nifungue mwamvuli labda mvua itanyesha,” alisema.

Alisema wasiwasi kuhusu chanjo umekuwa mkubwa hali ambayo wataalamu wa afya wanatakiwa kutoa maelezo zaidi ili wananchi waelewe.

“Lakini hizi chanjo zimepita hatua mbalimbali, hatua ya kwanza zilikuwa 184 zikapunguzwa zikabakia 35 zikapunguzwa zikabaki 34,zikabaki 27 leo zinazotumika ni chanjo tisa. Hivyo Ingekuwa ni haraka, leo zingekuwa 100 kwa sababu tulianza na 184 katika majaribio ila leo ziko tisa hivyo wanavyosema imeenda haraka si kweli,”alifafanua.

Akizugunguza kuhusu kuganda kwa damu alisema “Mfano astrazenec walivyotoa dozi milioni moja, watu wanne walipata kuganda damu. Ukitazama kwa asilimia hiyo ni 0.004.”

Chanzo: www.habarileo.co.tz