Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna uhusiano wa chanjo ya saratani shingo ya kizazi na ugumba

Mirija Hakuna uhusiano wa chanjo ya saratani shingo ya kizazi na ugumba

Fri, 18 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daktari Bingwa wa Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dk Caroline Swai ametaja saratani ambazo zinaongoza nchini kuwa ni shingo ya kizazi, matiti na tezi dume na kusema takwimu za wagonjwa wa saratani nchini mwaka 2020 ilikuwa ni takribani wagonjwa 10,000.

Amewataka wananchi kufanya vipimo mara kwa mara na kusisitiza kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi na ugumba kwa wasichana.

Hayo amezungumza jana mkoani Dar es Salaam, kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu ugonjwa wa saratani juu ya utekelezaji wa mradi mtambuka wa saratani (TCCP).

Dk. Caroline amesema jamii inahitaji kuendelea kupata elimu na namna ya kujikinga na maraddhi hayo akibainisha dalili zake kuwa ni uvimbe, maumivu, kutapika, uchovu kwa baadhi ya watu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live