Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna mgonjwa wa Omicron- Waziri Mkuu

Kassim Majaliwa?fit=749%2C537 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Sat, 11 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameitaka sekta binafsi kuitetea nchi kwa kuwa vita ya kibishara ni kubwa ikiwemo baadi ya watu kuitangaza Tanzania kuwa ni moja ya nchi hatari za kutembelea kwa madai ya kwamba wimbi la nne la kirusi cha Omicron limeshaingia.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 11, 2021, jijini Dar es Salaam, wakati wa kongamano la biashara na uwekezaji.

"Juzi hapa mmesikia tena, Tanzania ni nchi hatarishi kwa ugonjwa mpya wa wimbi la nne, sisi hatuna mgonjwa hata mmoja wa wimbi la nne hospitali, yote hiyo ni vita ya kibiashara kwahiyo sekta binafsi mtusaidie kusema haya, tukiacha watu wanapotosha wanaharibu nchi," amesema Waziri Mkuu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live