Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Hakuna gharama za uchunguzi wenye dalili kifua kikuu’

Wagonjwa TB ‘Hakuna gharama za uchunguzi wenye dalili kifua kikuu’

Fri, 25 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema imefuta gharama za uchunguzi kwa wagonjwa wote wenye dalili za kifua kikuu, li waweze kupata huduma hiyo kwa urahisi na kufikia lengo la kutokomeza ugonjwa huo, ifikapo mwaka 2030.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 24, 2022 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani, ambapo kitaifa yamefanyika viwanja vya Tangamano, Tanga.

Alisema takwimu zinaonesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2021, kulikuwa kuna wagonjwa takribani 47,000, ambao hawakufikiwa na huduma, hivyo bado wapo kwenye jamii na wanaendelea kuambukiza wengine.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya Ukimwi, Fatma Taufiq, amesema wataendelea kuishauri serikali kuendelea kutoa huduma za matibabu bure karibu na wananchi, ili wagonjwa wengi waweze kupata huduma bora kwa wakati.

Naye Meneja Miradi kutoka Shirika la Amref, Aisa Muya ameishauri serikali kuona namna bora ya kushirikisha wadau mbalimbai katika mapambano ya ugonjwa huo, ili iweze kuutokomeza ifikapo mwaka 2030.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mngandilwa, amesema kuwa katika kuimarisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa kifua kikuu, wameweza kununua hadubini 83, ambazo zimewekwa vituo vya afya tofauti mkoani humo, pamoja na kusogeza huduma katika vituo 315.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live