Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gwajima ataka kasi matumizi tiba asili

8a44e2f80b260282e23a8148bfd21607 Gwajima ataka kasi matumizi tiba asili

Sat, 27 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dorothy Gwajima amesema umefi ka wakati wa kuzalisha tiba asili kwa pamoja, kwa kuwa na viwanda na kufanya utafi ti ili kuinua bidhaa za tiba hiyo.

Alitaka kuwe na kamati itakayoharakisha kuwa na jukumu la pamoja la tiba asili katika kuzuia magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza.

Aliyasema hayo baada ya kuwatembelea wazalishaji wa bidhaa za tiba asili za NIMRCAF, Uzima Herbal Drops, FUKIZA UDANOL, Bingwa Mixed Spices na Bupiji zote za jijini Dar es Salaam.

“Tiba asili ilikuwepo tangu muda mrefu toka miaka ya 1990 na ilishaandikwa kwenye maandiko ya wizara pamoja na Sera ya Afya ya mwaka 2007 hivyo bidhaa zote zilizotengenezwa na wataalamu wa tiba asili ni kuwa na nia ya kuitafuta tiba kama nchi kwa njia yeyote”alisema.

Dk Gwajima alisema changamoto za kupumua zinawapata watu wengi, hivyo nchi inatakiwa kuwafikia wananchi wote na kwa rika zote kuanzia watoto wa shule ya msingi na wajengewe mazoea na uelewa kwamba lishe bora ni ipi na msingi wake uanzie tangu utotoni.

“Ninawatambua wazalishaji wote wa tiba asili na watoa huduma ambao wamesajiliwa na Baraza la Tiba Asili/ Mbadala, tutaendelea kuwatembelea wote kisha tutakuja na kikao cha kujumuisha mafanikio na changamoto zote pamoja na vyuo vyetu vikuu ambavyo vinafanya utafiti na taasisi zetu ili tuwe na njia ya kwenda mbele na kwa haraka pamoja na tutekeleze Ilani ya Uchaguzi ya kuwa na viwanda vya kuzalisha tiba asili na kuwa na utafiti endelevu unaotafiti mimea yetu ya nchi iliyobeba baraka za tiba asili ili Watanzania wanufaike” aliongeza Dk Gwajima.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye alisema chuo hicho kipo tayari kusaidia tafiti ili kuwe na matokeo chanya kwani wao wanamilikiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo matarajio yao ni kuongeza thamani ya tiba asili.

Mzalishaji wa mafuta tete ya Bupiji, George Buchafwe alisema mashine ya kujifukiza (SAUNA) inasaidia watu wote wanaoumwa na wasioumwa. Alisema huduma hiyo inasaidia kutoa jasho ambalo limebeba sumu na hivyo kumwezesha mtu kujenga kinga ya mwili.

Chanzo: habarileo.co.tz