Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Faini 50,000/- kwa baba, familia itakayochelewesha mjamzito hospitali

Db5c3d73871b768dd18c517a3598a5ca.jpeg Faini 50,000/- kwa baba, familia itakayochelewesha mjamzito hospitali

Sat, 30 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mama mjamzito atakayechelewa kwenda hospitali hadi kufikia kujifungulia nyumbani na atakayechelewa kuanza kliniki zaidi ya miezi mitatu toka apate ujauzito mume au familia italazimika kulipa gharama ya shilingi 50,000/- kwa serikali ya Kijiji.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema hayo leo wakati akiwasilisha taarifa ya Mpango wa Maendeleo ya Mkoa wa Mtwara 2021/2022 kwa katika kikao Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara.

Akielezea kuhusu malengo ya muda mfupi kuhusu mpango wa maendeleo wa kwenye sekta ya Afay, Gaguti amesema mkoa umepanga mpango wa muda mfupi kupunguza vifo vya akina mama wajazito na watoto wakati na baada ya kujifungua kwa asilimia 50 toka vifo sita kwa mwezi hadu tatu mwaka 2012/22 hadi 2024/25.

Amesema mpango huo utasimamiwa na wakurugezi wa halmashauri pamoja na watendaji wa halmashauri hizo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz