Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu madhara yatokanayo na kemikali kwenye vipodozi

73063 Vipodozi+pic

Tue, 27 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kama unadhani kuwa mrembo lazima utumie vipodozi vyenye kemikali unajidanganya, ukweli ni kwamba vipodozi vina kemikali ambazo zinaweza kuharibu mfumo wa uzazi kwa mwanamke ambapo anaweza kuzaa mtoto mwenye mtindi wa ubongo.

Hayo yamebaika jana Jumatatu Agosti 26,2019 wakati wa uzinduzi wa Chama cha Urembo na Vipodozi Tanzania (TCA) jijini Dar es Salaam nchini Tanzania wenye lengo la kuwakutanisha wauzaji, wasambazaji na watengenezaji bidhaa za urembo kuwa na sauti moja kwa ajili ya kukuza sekta hiyo.

Katika hafla hiyo mkurugenzi kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa Serikali ya Tanzania, Sabanitho Mtega alisema zaidi ya watu 335,000 hufa kila mwaka kwa ajili ya kujihusisha na matumizi ya kemikali duniani.

Kufuatia takwimu hizo mkurugenzi huyo alisema ipo haja ya kuainisha njia madhubuti kwa ajili ya kuzuia madhara yatokanayo na kemikali kwa jamii na mazingira kwa ujumla.

“Ukiangalia hiyo idadi ni kubwa sana, tunaposema kukuza uchumi wa nchi tunahitaji kuwa na watu wenye afya lakini pia kuwa na mazingira salama hivyo hatuna budi kuwa na njia za kuzuia matumizi ya kemikali kiholela,” alisema.

Alisema Serikali inaendelea kudhibiti kemikali hizo kwa kuhakikisha  kila anayesafirisha au kuingiza kemikali ndani ya nchi anasajiliwa na kupewa cheti cha kufanya biashara hiyo huku lengo likiwa kuzuia kemikali hiyo isiweze kuleta madhara.

Pia Soma

“Kwa hiyo niendelee kutoa rai kwa wajasiriamali wa vipodozi tunaotumia kemikali kuzalisha bidhaa hizo zinakuwa zile zisizokuwa na madhara kwa wananchi na hakikisheni mabaki ya kemikali mnayatupa bila kuathiri mazingira kwani baadhi ya vipodozi huwekwa kemikali kama dawa ambayo kazi yake ni kutibu lakini ikitumika kinyume na utaratibu inaleta madhara,” aliongeza mkurugenzi huyu.

Kwa upamde wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu aliwataka wazalishaji wa vipodozi kuzalisha bidhaa zinazolenga kulinda na kuimarisha afya ya jamii.

“Tengenezeni bidhaa za urembo ambazo hazina madhara kwa jamii, viambata vyenye sumu vina madhara katika afya zetu, lakini pia msiwafiche wale wanaotengeneza vipodozi vyenye viambata sumu wafichueni na sisi tutawachukulia hatua kali za kisheria,” alisema.

Alisema vipodozi vyenye viambata sumu vina madhara makubwa katika jamii ikiwemo magonjwa ya saratani, ini na figo hivyo mnapotengeneza vipodozi zingatieni afya.

“Sasa hivi tunaona ongezeko la magonjwa ya saratani, ini na figo mfano katika takwimu zilizotolewa na Taasisi ya Saratani (Ocean Road) zinaonyesha kuwa ugonjwa huo umeongezeka kutola watu zaidi ya 2,000 wenye saratani mwaka 2005 hadi watu 7,649 huku sababu moja wapo ikiwa matumizi ya vipodozi vyenye kemikali,” alisema Ummy.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz