Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu kuhusu maumivu ya mgongo kwa wanawake

Maumivu Mgongo (22).jpeg Fahamu kuhusu maumivu ya mgongo kwa wanawake

Sat, 25 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maumivu ya kiuno ni tatizo linalosumbua wanawake wengi mara kwa mara. Hujitokeza hasa wakati wa hedhi kisha kufifia.

Kuna maumivu ya kiuno ambayo hukaa kwa muda mrefu kati ya miezi mitatu mpaka miezi sita na kuendelea au kuwa yanajirudia mara kwa mara.

Maumivu haya huweza kusababishwa na matatizo kwenye via vya uzazi, kibofu cha mkojo, utumbo mkubwa au misuli ya nyonga.

Yanaweza kuwa yanaendana na mzunguko wa hedhi au la, huwa mara nyingi chini ya kitovu na kiunoni. Maumivu yanaweza kuwa makali kiasi cha kuathiri shughuli za kila siku.

Kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha mwanamke kupata maumivu ya kiuno kwa muda mrefu, sababu hizi ni kuwa na maambukizi ya ndani ya kiuno ya muda mrefu Chronic Pelvic Infection.

Maambukizi haya hutokana na ugonjwa wa Kifua Kikuu na huweza kusababisha maumivu ya kiuno.

Wengine huumwa kiuno kutokana na seli za ukuta wa uzazi kuota sehemu nyingine za uzazi. Huleta maumivu wakati wa hedhi au kufanya mapenzi hali hiyo kitaalam huitwa Endometriosis.

Wanawake wengine hali hiyo husababishwa na maambukizi ya muda mrefu ya shingo ya uzazi au mji wa uzazi na husababisha maumivu ya kiuno wakati wowote na wakati wa kufanya mapenzi.

Wengine huumwa baada ya mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi, kitaalam huitwa Ectopic Pregnancy au kuwa na uvimbe wa kizazi Uterine fibroids ambao husababisha maumivu pale ambapo unakua kwa haraka na kukandamiza kiungo kingine.

Dalili nyingine ni kukojoa mara kwa mara, kukojoa usiku na kushindwa kubana mkojo.Ugonjwa wa kidole tumbo Chronic Appendicitis pia ni dalili. Tatizo la kidole tumbo huleta maumivu upande wa kulia chini ya kitovu ambayo huwa hayatulii kwa dawa za maumivu.

Kusagika kwa mifupa kwenye maungo huweza kusababisha kuumwa kiuno. Mifupa ya maungo ya kiuno inaposagika, husababisha maumivu makali maeneo ya kiunoni hasa wakati wa kutembea.

TIBA: Maumivu ya kiuno ya muda mrefu hutibiwa kwa kugundua chanzo cha maumivu kwanza, kujua historia ya tatizo, uchunguzi pamoja na vipimo hufanyika. Matibabu hutegemea na chanzo cha tatizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live