Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu jinsi ya kuponya katika maisha ya mwanadamu

66724 Mahubiri+pic

Sun, 14 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Wiki iliyopita nilifundisha kuhusu uponyaji wa kiungu, leo tujifunze jinsi ya kuponya. kwanza lazima ieleweke kwamba kuna tofauti kati ya uponyaji na mponyaji, uponyaji ni kipawa cha Mungu mponyaji ni mtu wa Mungu.

Mathayo 10:1, imeandikwa Mungu aliwapa mamlaka ya kuponya magonjwa yote, baadaye aliwaagiza akisema ponyeni wagonjwa toeni pepo fufueni wafu takasani wenye ukoma mmepata bure toeni bure.

Hasemi niombeni nije kuponya bali anawaagiza akisema ponyeni, hii ina maana kwamba yeye amewapatia uponyaji wake ili wao wakawaponye watu wake. jambo lililofichwa hapa ni jinsi gani tuponye, hilo ni siri yake Mwenyezi ambayo huifunua tu kwa mjumbe wake aliyemtuma na kumpa karama ya uponyaji saa hiyohiyo anapotimiza wajibu wake kwa utukufu wa Mungu.

Kwa fano Biblia inasema: Naamani alipokuwa na ukoma alimwendea Nabii Erisha, Biblia haionyeshi popote kwamba Erisha alimuombea Naamani bali inasema alimwambia akajichovye kwenye mto Yorodani alipojichovya akawa mzima aliponywa ugonjwa wa ukoma.

Naamani alikuwa anaamini ataponywa na Mungu lakini hakujua njia gani itatumika kumponya siri hiyo alikuwa nayo Erisha peke yake. Mungu akikupa kipawa anakupatia na njia za kipawa kutimiza makusudi yake, mfano mwingine ni kipofu aliyekutana na Bwana Yesu, Yesu alitema mate chini akatengeneza tope kwa yale mate akampaka kipofu machoni kisha akamwambia kanawe aliponawa akapata kuona.

Wazia hilo, Yesu aliandikiwa kwamba atawafumbua vipofu macho lakini haikuandikwa jinsi gani atawafumbua ilikuwa siri ya Mungu ndani yake ambayo ilikuwa lazima ifunuliwe katika siku ya kipofu kwa ajili ya kipofu. Unaona! Leo watu wanajiuliza maswali mengi wanapoona baadhi ya watumishi wanatumia vitu kama maji, chumvi, mafuta nk. kuponya watu na wanadhani wamepotoka, suali la msingi siyo vitu anavyotumia mtu maana hata Musa alitumia fimbo na nyoka wa shaba kutimiza miujiza ya Mungu, muhimu ni baada ya matumizi ya vitu hivyo nini kimetokea kilichotarajiwa? Maana imeandikwa akitokea mtu kwenu akasema yeye ni nabii msikilizeni kama maneno yake yatatimia basi atathibitika mwaminini mtu huyo, leo Dunia imejaa uwoga kwa sababu wengi wanaojaribu kuponya watu hawana karama za kuponya hivyo Mungu hawezi kugharimia mafunuo kwenye huduma zao, sasa wakikosa matokeo ya uponyaji wanaanza kuchukua tahadhari dhidi ya waliopewa neema na mwenyezi Mungu. Japo si vibaya kuwa makini na waponyaji hawa maana ibilisi naye anaweza kuwachomeka matapeli humo, ndiyo maana imeandikwa msiziamini kila roho bali zijaribuni hizo roho kwamba zinatokana na Mungu au la! Biblia inasema mmepata bure toeni bure ukikutana na mtu anauza kipawa cha Mungu, basi ujue umekutana na shetani, Isaya 55: Imeandikwa njooni nunueni bila fedha wala bila thamani. Nafikiri imani yako haina shaka tena juu ya uponyaji wa Kiungu, wazia inavyosema Biblia juu ya mitume na manabii waliotangulia, Ebrania 11: ...haisemi Mungu alisimamisha jua bali inasema kwa imani Joshua alisimamisha jua.

Pia Soma

Mahali pengine haisemi Mungu alimfufua Dorkas bali inasema Petro akamwambia yule maiti amka akaamka. Hiyo inaonyesha uhai ni wa Mungu anayefufua ni mtu aliyetumwa kufufua ndiyo maana Petro alipomponya kiwete watu alitaka kumwita Mungu, yeye akapiga kelele na kusema mimi siyo Mungu bali ni shahidi wake kwamba yule mliyemsulubisha yu hai nasi kwa uwezo wake tumefanya haya. Yohana 14:1 ...Bwana Yesu alisema kazi hizi ninazozifanya ninyi nanyi mtazifanya naam, na kubwa kuliko hizi mtazifanya, hasemi nitawafanyia anasema mtazifanya ninyi wenyewe.

Bwana ametupatia kazi za kufanya kazi za kuihubiri Injili na kuponya na atatufunulia jinsi gani tuwaponye, katika huduma yangu hapa Yespa Kihonda Morogoro mjini uliza kwa Nabii Joshua. Mungu amenitumia kuponya watu wenye magonjwa ya kila aina, mikosi na mabalaa maskini wamekuwa mamilionea sifa na utukufu vimrudie yeye aliye juu Mwenyezi. Basi sasa nakushauri ondoa shaka njoo kwa Mungu kwa imani yako utapata rehema na uponyaji bure, kwa uponyaji tuma neno.

“Uponyaji” kwa njia ya WhatsApp kwenda namba 0742 121 212 Muujiza utakufuata popote ulipo. Amen.

Chanzo: mwananchi.co.tz