Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu haya kuhusu uchangiaji damu

Blood Donation Fahamu haya kuhusu uchangiaji damu

Tue, 14 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kila ifikapo June 14 duniani kote huwa ni siku ya kuchangia damu duniani yaa 'World Blood Donor Day' lenye lengo la kuifahamisha dunia umuhimu wa kuchangia damu pamoja na kuhamasisha watu kuchangia kwa hiari.

Uhamasishaji huu hufanyika kwa mtu mmoja mmoja,Taasisi, mashirika mbali mbali n.k katika kuchangia damu ili kusaidia uwepo wa Damu ya kutosha kwenye vituo vya afya nchini kote.

Ikumbukwe kuwa damu ni Uhai, hivo ukichangia Damu umesaidia kumpa mtu uhai lakini pia Uhitaji wa damu bado ni mkubwa sana sio kwa TANZANIA pekee bali kwa Dunia nzima kwa Ujumla.

Watu mbali mbali huhitaji damu duniani kote kutokana na Sababu mbali mbali ambazo husababisha Damu kupungua Mwilini kama vile, ajali, Vita, Wajawazito wanaojifungua Watoto wanaopata shida ya Anemia, Uwepo wa magonjwa mbali mbali kama vile; Malaria, Sickle cell n.k Matatizo ya damu kushindwa kuganda au Damu kutokugand, Matatizo kama blood and bone marrow disorders, inherited haemoglobin disorders na Wagonjwa ambao wapo kwenye tiba kama vile upasuaji wa aina mbali mbali N.K

Hivo basi, Katika kumbana na Tatizo hili la ukosefu wa Damu, huku mahitaji ya damu yakiongezeka kila Leo,

Dunia ikiwemo Tanzania imeamua kuanzisha mikakati mbali mbali ya kupambana na tatizo hili, Zipo kampeni na program mbali mbali ambazo zinaendeshwa kila kona ili kusaidia kutatua tatizo hili. Kauli mbiu ya uchangiaji damu mwaka huu ni “Donating blood is an act of solidarity. Join the effort and save lives”

Lengo lake ni kuendelea kuhamasisha watu zaidi kuchangia Damu kwa hiari ili kuokoa maisha kwenye jamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live