Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu faida za kutoa machozi kwenye maisha

Msaikolojia Fahamu faida za kutoa machozi kwenye maisha

Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: eatv.tv

Kupitia kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio Mwanasaikolojia George Boniphace amesema kutoa hisia zako kwa njia ya kutoa machozi kuna faida kubwa kwenye mwili wa binaadam.

"Watu tunatakiwa tujifunze kutoa hisia zetu kama kusikia huzuni, wivu, chuki au upendo tafuta njia ya kuvitoa, takwimu zinasema sababu zinazofanya wanawake kuishi sana ni kutokaa na vitu ambavyo wasipovizungumza basi watalia kwa hisia" 

"Kulia kule kwa hisia mtu anakuwa anatoa hasira vinyongo hivyo inamsaidia kujenga mwili wake kuwa mpya na kupata experince nyingine kwa wanaume hali hiyo haitukuti sana kwa sababu kuna jamii zingine zinaamini mwanaume akilia ni udhaifu" ameongeza Mwanasaikolojia George Boniphace.  

Chanzo: eatv.tv