Kama sio mjamzito au upo chini ya miaka 18 usisome makala hii.
Kuna watu walikuwa hawaamini kama unaweza kufanya tendo la ndoa ukiwa na ujauzito. Mwanamke akiwa na mimba anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa hata kama anatarajia kuzaa kesho yake.
Hakuna tatizo linalomzuiya kufanya hivyo,, baadhi ya wanawake wamekuwa wazito sana kufanya hivyo kwa kuwa na sababu mbalimbali na uoga mwingi. Bila ya kutambua kwamba wanazikosa faida hizi.
Faida zenyewe ni kama zifuatazo.
1. Husaidia uchungu mzuri, na kupona mapema :kufika kileleni kwa wakati wa tendo la ndoa huambatana na kubana kwa misuli ya nyonga hii husaidia kuweka imara misuli ya nyonga ambayo ni muhimu sana wakati wa kusukuma mtoto na baada ya kuzaa.
Maana misuli hii ikiwa legevu au kutokuwa imara,mwanamke huweza kushindwa kuzaa kwa njia ya kawaida na hata baada ya kuzaa huweza kushindwa kuzuiya haja ndogo (mkojo) usitoke wenyewe au kuvuja damu kwa mda mrefu sana.
2. Hupunguza kwenda hovyo kutoa haja ndogo (kukojoa au kujikojolea) Wakati wa ujauzito mtoto anapo zidi kua mkubwa anazidi kukandamiza kibofu cha mkojo,hii humfanya mwanamke mwenye ujauzito aende chooni mara kwa mara, wakati mwengine hata akipiga chafya au kukohoa basi mkojo unaweza kutoka wenyewe,. Tendo la ndoa huibana misuli ya nyonga na kuzuiya hali hii.
3. Huzuiya uwezekano wa kupata kifafa cha mimba. Tafiti zinaonyesha kwamba aina ya protini inayopatikana kwenye mbegu za mwanaume huongeza kinga mwilini mwa mwanamke na kuzuiya uwezekano wa kupata kifafa cha mimba, ambacho kinaua wanawake wengi sana.
4. Hutibu tatizo la kufika kileleni kwa shida, Kipindi cha ujauzito chuchu za mwanamke na kinembe chake huvimba na kuongezeka hisia maradufu huku kiwango cha homoni na Oestrogen kikiwa juu sana. Hii humfanya kufika kileleni kirahisi sana kuliko mwanzoni.
5. Huwapa uwezo wa kujiamini:.. Kipindi cha ujauzito mwanamke hupata hofu sana na kutojiamini na mwili wake,, hupata wasiwasi kwamba mwili wake unaharibika , hivyo kitendo cha mwanaume wake kuendelea kushiriki tendo la ndoa naye humpa kujiamini kwamba mwili wake bado uko kwenye hali nzuri na anapendwa.
6. Hupunguza msongo wa mawazo:,, Kipindi cha ujauzito wanawake wengi huwaza sana kuhusu kesho yao, (kwa mfano,… Je swala la uchumi litakuaje?, mwili wangu utakuaje,, Je nitapa jinsia ninayoitegemea? Na kadhalika) Tendo la ndoa hutoa homoni ya upendo kwa jina la Oxytocn, homoni hii hupunguza mawazo na humpa amani mjamzito.
7. Huongeza upendo na mshikamano kati ya wapenzi:,,, Katika hali ya kawaida wanandoa wakikwazana wanaweza wakapatana kwa kushiriki tendo la ndoa tu. Amani na upendo kipindi hiki ni muhimu sana, kwani kuna mtoto anakuja ambaye anatakiwa kuzaliwa huku baba na mama wakipatana kwa umoja.
8. Hukuanda na uchungu:.. Ukishiriki tendo la ndoa wakati wa tarehe zilikadiriwa zimefika unapata homoni moja, kutoka kwa mbegu za mwanaume kwa jina la Prostglandin.. Homoni hii huivisha mlango wa uzazi na kuanza kufunguka taratibu kujiandaa na uchungu.
9. Hutibu tatizo la kukosa usingizi: Wanawake wengi wajawazito huwa na dalili mbalimbali za maumivu, na kuumwa sehemu tofauti za mwili na msongo wa mawazo,, hii inaweza kuwakosesha usingizi kabisa…. Tendo la ndoa huweza usingizi mzuri.
10.Hupunguza presha ya damu:….Kipindi cha tendo la ndoa Presha ya damu hushuka kwenye kiwango kizuri sana. Hii ni muhimu sana kwa wanawake wenye hatari ya kupata kifafa cha mimba , kama wanene sana,, wenye kisukari, au wenye historia za ugonjwa wa presha kwenye koo zao.
Mwisho:.. Hakikisha unatumia staili za tendo la ndoa ambazo hazimuumizi mama au mwana,. Yani hakikisha haulalii tumbo lako hasa mimba ikiwa kubwa. Kuna staili muhimu kipindi hiki kwa mwanamke mjauzito. Mfano (kama kulala upande mmoja kisha unauwenua mguu mmoja, au kuukalia taratibu kisha kufany tendo la ndoa.