Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu! Wanasayansi walitengeneza dawa ya nguvu za kiume kimakosa?

Nguvu Za Kiume Mn Je wajua, dawa za nguvu za kiume ziligunduliwa bahati mbaya?

Sun, 12 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAMA HUJUI BASI HAPA UTAJUA KILA KITU! Unafahamu kama dawa aina ya Viagra ilianza kuuzwa mnamo 1998 na ilivyoingia sokoni tu ikafanya vizuri mara moja?

Iligunduliwa na kampuni ya utengenezaji dawa dawa Pfizer, "kidonge cha bluu" ikazalisha pesa za kutosha. Katika miezi mitatu ya kwanza pekee, Wamarekani walitumia wastani wa dola milioni 400 kununua dawa ya kukosa nguvu za kiume.

Haikuchukua muda mrefu kwa sekta hiyo kuweka malengo yake katika nusu nyingine ya soko, upande wa wanawake, na kuona fursa ya kuongeza faida yake maradufu.

"Nilianza kusoma fiziolojia ya kijinsia wakati Viagra ilipokuja. Na hisia ilikuwa kwamba wakati huo, pesa nyingi zilianza kuingia katika utafiti wa ngono," anakumbuka Nicole Prause, mwanasayansi na mtafiti katika Chuo Kikuu cha California, Los Angeles (UCLA).

Hatujawahi kuona chochote cha ukubwa huu. Sayansi yetu [fiziolojia ya ngono] bado imetengwa kwa kiasi fulani, inachukuliwa kuwa eneo hatari. Kuna kampuni nyingi ambazo hazitaki hata kuwa karibu na mada hii."

Lakini takriban miaka 25 na mamilioni mengine mengi ya dola yaliyofuata baadaye, tasnia ya dawa haijawahi kupata toleo la "kidonge cha bluu" kwa ajili ya wanawake.

Kushindwa huko, kumefungua nafasi kwa mjadala mpana juu ya masuala ya kujamiiana kwa upande wa wanawake, pia ni inahusisha simulizi kuhusu miiko na imani potofu kuhusu hamu ya wanawake kwenye tendo la ndoa, kama ilivyoangaziwa na wataalam.

Historia ya utafutaji wa "kidonge cha pinki"

Historia ya 'viagra' ama dawa za kuongeza nguvu za kiume inajulikana sana.

Dawa inayotumiwa leo kwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume iligunduliwa kwa bahati mbaya: "Tulikuwa tukitengeneza dawa ya angina, tatizo la moyo," Dkt. Mitra Boolell, ambaye alifanya kazi katika idara ya utafiti ya Pfizer nchini Uingereza, anaiambia BBC Brazil.

"Wakati huo baadhi ya washiriki wa majaribio ya kliniki walianza kuripoti kuwa nguvu za kiume zaidi kuliko kawaida. Hapo awali hatukuzingatia sana, tulifikiri ni kwa sababu washiriki walikuwa vijana."

Pfizer ni miongoni mwa makampuni makubwa ya dawa duniani ambayo yanafanya tafiti kubwa za madawa na hivi karibuni walikuwa miongoni mwa makampuni yaliyotengeneza chanjo ya Covid-19 ambayo nchi nyingi za Afrika zimeitumia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live