Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FCS kuchangia damu MNH

25626 Damu+pic TanzaniaWeb

Tue, 6 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa damu, Mfuko wa Asasi za Kiraia (FCS) umejipanga kuadhimisha siku ya kimataifa ya utoaji kwa kuchangia damu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS,  Francis Kiwanga akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Novemba 5, 2018 amesema lengo la siku hiyo linavyoelekeza, wafanyakazi wa mfuko huo wameamua kutumia siku hiyo kuchangia damu ili kunusuru maisha ya watu ambao wako hospitalini wakisubiri kupata huduma hiyo.

Amesema siku hiyo ambayo inafahamika kama Jumanne ya utoaji huadhimishwa katika mataifa 10 na hivyo Novemba 24, 2018 wafanyakazi wa FCS watajitolea kuchangia damu.

Pamoja na kuchangia damu, FCS pia imejipanga kufanya mambo kadhaa kuanzia leo hadi Novemba 27 ikiwemo kutembelea kituo cha kulelea watoto cha New Hope For Girls.

Amesema ili kuhakikisha vijana nao wanakuwa na utamaduni huo, taasisi hiyo itaendesha kampeni maalum kwa lengo la kuwazawadia vijana wanaosaidia jamii zao.

“Kupitia kampeni hii, tunawakaribisha vijana ambao wamefanya jambo lolote kwa ajili ya jamii zao na kuleta mabadiliko au kutatua changamoto fulani watuletee stori zao tutazishindanisha na mshindi wa kwanza atapata dola 1,500,” amesema.

“Utoaji huu si lazima iwe fedha inaweza kuwa muda, kupaza sauti kwa ajili ya wanyonge au nguvu kazi katika miradi ya kijamii.”

“Ukiona umefanya lolote tuandikie kisa chako kwa maneno yasiyozidi 200 tutumie na pia uiweke kwenye akaunti yako ya mtandao wa kijamii ikiwa na hashtag UtoajiWanguHazinaYangu,” amesema Kiwanga.

Chanzo: mwananchi.co.tz