Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Elewa hili kusuhu usugu wa dawa..

Dawa Sumuuu Elewa hili kusuhu usugu wa dawa..

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mratibu wa usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa kutoka Wizara ya Afya Emiliana Fransic amewataka madereva wa vyombo vya usafiri kutoa elimu kwa abiria kuhusiana na matumizi sahihi ya dawa ili kuepukana na Usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa.

Emiliana ameyasema hayo katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Roll Back Antimicrobial Resistance Initiative (RBA Initiative) kwa madereva wa vyombo vya moto juu ya matumizi sahihi ya dawa yaliyofanyika mkoani Dodoma

“Usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa hutokea pale ambapo vimelea hivyo hubadilika na kuwa sugu kwa dawa zinazotumika kwa matibabu ya magonjwa ya kuambukiza hivyo wajibu wetu ni kutumia dawa zilizotolewa na wataalamu wa afya”. Amesema Emiliana.

Aidha amesema ili kuimarisha kinga za mwili vizuri ni vyema kwa kila mwananchi atumie dawa baada ya kufanya vipimo na kuthibitishwa na waatalamu wa afya ili kutoingia katika usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa.

Hata hivyo Emiliana amesisitiza utolewaji wa elimu kupitia vyombo vya usafirishaji kwani madereva hao ni miongoni mwa watu muhimu kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya kupambana na usugu wa vimelea wa magonjwa dhidi ya dawa.

Pia, amesisitiza juu ya matumizi sahihi ya dawa ikiwa ni Pamoja na kutokatisha dozi pale unapojisikia nafuu, kutompa mgonjwa dawa zako Pamoja na kuzuia maambukizi kwa kunawa mikono mara kwa mara

Chanzo: www.tanzaniaweb.live