Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Drone za kusambaza dawa kuanza majaribio

Drone Za Kusambaza Dawa Kuanza Majaribio Drone za kusambaza dawa kuanza majaribio

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: millard

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Serikali imekamilisha kuingiza vituo vyote kwenye mfumo wa kuhifadhi taarifa zote za vituo kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Taifa ili kuufanyia majaribio na pia kutazama gharama za usafirishaji dawa kupitia mfumo wa ndege maalum (drones) ukilinganisha na usafirishaji kwa njia ya magari ili maamuzi sahihi yafanyike.

Dkt. Mollel amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati akijibu swali Namba 83 kwa niaba ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ambapo swali hilo limeulizwa na Mbunge wa Kilindi, Omari Mohamed Kigua aliyeuliza “Je, ni lini Serikali itatumia Drones kusambaza Dawa katika Zahanati zetu Vijijini”

Dkt. Mollel amesema Serikali ilishakamikisha mfumo ambao unahifadhi taarifa zote za vituo kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Taifa, Mfumo huu utasaidia kupata taarifa za kijiografia (Geo coordinates) za vituo vyote Nchi.

Chanzo: millard