Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dr. Gwajima azindua kamati ya Utalii wa Matibabu

31ef88dc5a171c0f5bd2e277c0d41fb6 Dr. Gwajima azindua kamati ya Utalii wa Matibabu

Tue, 13 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii jinsia,Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima amezindua rasmi kamati itayoshughulikia matibabu ya utalii nchini.

Mpango wa utalii wa matibabu (Medical Tourism) unalenga kufikia nchi zote Duniani ikiwa ni hatua za kutumia huduma za kibingwa zinazopatikana ili kuingiza kipato zaidi.

Miongoni mwa Huduma hizo za kibingwa zilizolengwa ni zile zinazopatikana katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road,Taasisi ya Tiba ya Mifupa(MOI),Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH).

Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo iliyohusisha watu 15 kutoka taasisi mbalimbali,Do Gwajima amesema hatua hiyo itasaidia ukuaji uchumi na uboreshwaji zaidi wa sekta ya afya na zingine.

“Kwa wataalamu tulionao na miundombinu tumeona tufanye ‘medical tourism’,maana yake mtu anaweza kuja kutibiwa tu kwasababu anajua kuwa kuna huduma anayotaka au anaweza kuja kwa lengo la utalii na kuona kuwa apime afya au kutibiwa kwasababu nchi yetu inauwezo huo .

“Tumezindua kamati rasmi na inaanza sasa safari matumaini yetu ni kwamba uwekezaji uliofanywa katika sekta ya afya tuna deni la kurejeshea serikali mapato ili ikasaidie sekta nyingine ,Lazima tutumie fursa zilizopo kama ni ndege tunazo , teknolojia ipo sasa ,wataalamu wapo na huduma zipo ,”alibainisha.

Dk Gwajima amesema licha ya kuwepo kwa vifaa na wataalamu lakini pia huduma kwa wateja inatakiwa kuzingatiwa zaidi.

“Tunataka huu uwekezaji uanze kuleta matunda kwamba watalii kutoka Duniani wakija wapende sehemu hizi wakija wapime afya zao na kutibiwa tupate kipato iwe ni kwa bima na moja kwamoja itaingia kwenye mfuko wa serikali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Mohammed Janabi amesema kamati hiyo ambavyo itadumu kwa miaka minne imeweka mikakati mingi ili kuhakikisha Tanzania kuwa kituo bora cha utalii wa matibabu .

“Rais Samia alivyokuja alishauri utalii wa matibabu katika nchi yetu lakini pia tunataka watanzani wenyewe wajue huduma zetu na waje ,takwimu zinaonesha kuwa kwa mwaka 2013 watu waliotibiwa mje ya nchi ni 23.000 na gharama zilizotumika ni milioni 500.

“Tunataka sasa watanzania watibiwe hapa na tupate faida kutokana na huduma zetu,kikubwa tutakachozingatia ni unafuu wa bei kama tutatengeneza vifurushi yenye bei nafuu tutafanikiwa kwasababu nchi za SADC ni nchi chache sana zenye huduma kama hizi,”amesema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz