Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dr.. Gwajima ataka fedha za dawa vituoni ziheshimiwe

52c5d3057d84f5dc7743c016bf230a3e Dr.. Gwajima ataka fedha za dawa vituoni ziheshimiwe

Wed, 23 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amewataka viongozi wa vituo vya kutolea huduma za afya vya umma, kuheshimu fedha za dawa kadri zilivyopangwa kwenye bajeti ya serikali kuu na vyanzo vingine ili kuondoa kero ya upatikanaji wa dawa.

Alisema hayo katika ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Kutathimini Utekelezaji wa Vipaumbele vya Kisera katika Sekta ya Afya uliofanyika jijini Dodoma.

Alisema yapo malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu ukosefu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini, hivyo viongozi wa hospitali na vituo vya kutolea huduma vya umma wanapaswa kuanisha matumizi ya fedha za dawa walizopokea au kutoka kwenye makusanyo ya mapato ya hospitali na matumizi yake.

Aliongeza kuwa licha ya mafanikio ya sekta ya afya nchini, zipo changamoto zinazohitaji juhudi za pamoja kuzikabili ikiwamo ya wananchi wengi kuwa nje ya mfumo wa bima ya afya, hali inayowanyima wepesi wa kupata huduma za afya kwa wakati kutokana kutokuwa na kifedha.

Kwa mujibu wa Waziri Gwajima, hadi sasa ni asilimia 11 pekee ya Watanzania waliojiunga na huduma za bima ya afya.

Kuhusu tiba asili na tiba mbadala, Dk Gwajima alisema zimekuwa zikisaidia kutibu magonjwa mbalimbali na kwamba, serikali inakusudia kuimarisha kitengo cha utafiti wa tiba mbadala.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dk Festo Dugange, alisema: "Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii Iliyoboreshwa unachangia asilimia 5 ya wanufaika wote waliojiunga katika mifuko ya bima za afya nchini na katika kipindi cha utekelezaji kuanzia Julai 2018, tumefanikiwa kusajili kaya 557,882 sawa na wanufaika 3,347,112 kufikia Novemba 2020."

Hata hivyo amesema jumla ya shilingi bilioni 16.2 zimekusanywa katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2020 ambapo zimewezesha kuimarisha huduma za afya kwenye vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na kuwawezesha wananchi yakiwemo makundi maalum kuzifikia huduma hizo bila vikwazo vya kifedha.

Chanzo: habarileo.co.tz