Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dozi Laki 5 za Pfizer kuwasili nchini mwezi huu

Fc902a7c2f060d24bbe8f0e409372b64 Dozi Laki 5 za Pfizer kuwasili nchini mwezi huu

Sun, 17 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali inatarajia kupokea chanjo dozi 500,000 aina ya Pfizer mwishoni mwa mwezi huu, ambazo ni sehemu ya dozi milioni 3.7 za aina hiyo ya chanjo kuingizwa nchini kwa mpango wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wa Covax Facility.

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa leo Oktoba 17, wakati akitoa Taarifa ya Wiki ya Serikali jijini Mwanza na kudai kuwa majokofu ya baridi kali 14 yenye uwezo wa kuhifadhi chanjo zote milioni 3.7 yameshafungwa Dar es Salaam.

Aidha, Msigwa ametoa takwimu kuwa mpaka kufikia Oktoba 15, 2021 Watanzania 940,507 walikuwa wamepokea chanjo ya UVIKO-19, ambao sawa na asilimia 88.9 ya chanjo za awali 1,058,400.

Amesema kuwa shehena ya chanjo 1,065,000 aina ya Sinopharm zilizokuja kutoka China zimeanza kusambazwa katika Halmashauri na Mikoa yote.

Chanzo: www.habarileo.co.tz