Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt. Maboko: Wanaume wako nyuma kujitokeza kupima VVU

1 1.jpeg Dk. Leonard Maboko

Fri, 20 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, amesema watu 54,000 nchini wamepata maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa mwaka 2021 huku ripoti mpya ikibainisha kupungua kwa maambukizi hayo kulinganishwa na mwaka 2020 ambao watu 68,000 walipata maambukizi mapya.

Dk. Maboko, amesema hayo wakati wa ufunguzi wa semina kwa wahariri na waandishi wa habari aliporejeshwa ripoti mpya ya zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Ukimwi HIV/AIDS (UNAIDS).

Aidha amesema ripoti mpya inaonyesha juhudi zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau kukabiliana na VVU/UKIMWI zimekuwa na matokeo chanya.

Hata hivyo, mkurugenzi huyo amesema bado kunahitajika nguvu zaidi ili kuzuia maambukizo mapya ili kupunguza kasi ya maambukizo.

”Ukiangalia takwimu za vifo wanaume wanaongoza wakati wanawake wanaongoza kwa maambukizi hii inamana kwamba wanaume wako nyuma kujitokeza kupima na wako nyuma kutumia ARVs (dawa za kupunzuza makali ya VVU)” amesema Dkt. maboko

Dkt. Maboko amesema kuwa makadirio mapya yanaonyesha vijana wanaendelea kuwa kundi lililo hatarini zaidi dhidi ya VVU hivyo program nyingi sasa zimeelekezwa kwa kundi hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live