Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Temu: Ubora wa mtoto hautenganishwi na mama mjamzito

88741 Unicef+pic Dk Temu: Ubora wa mtoto hautenganishwi na mama mjamzito

Mon, 16 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jamii ya Kitanzania imetakiwa kutengeneza mazingira ambayo yatamuwezesha mama mjamzito kujifungua salama mtoto mwenye afya.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Desemba 16, 2019 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Shirika  la Amref Tanzania, Dk Florence Temu wakati wa kongamano kuhusu kaki za mtoto lililoandaliwa kwa pamoja baina ya Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (Unicef), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Dk Temu amesema hakuna namna ambavyo ubora wa mtoto unaweza kutenganishwa na afya ya mama hivyo ni muhimu kwa jamii kuweka mazingira yatakayomfanya mama kulea ujauzito na kujifungua salama.

“Takwimu za 2015 katika vizazi hai 100,000 wa mama 556 walikuwa wanafariki na watoto 45 wanafariki kati ya 1,000 wanaozaliwa.”

“Hii inaonyesha ipo haja ya kuendelea kuboresha huduma za afya ili anapotokea mama mjamzito basi apate huduma bora,” amesema

Dk Temu amesema suala la ujauzito sio la sekta ya afya peke yake ni muhimu kwa jamii kutambua kuwa ina wajibika katika kuhakikisha mama anakuwa salama wakati wote wa ujauzito hadi kujifungua.

Amesema hilo litawezekana kwa kuweka na kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwamo kusogeza karibu huduma za afya na kuwaongezea uwezo wakunga.

Asilimia 85 ya uzazi ni wa kawaida wala hauhitaji hata mkunga au muuguzi ambaye amebobea. Mkunga mwenye ujuzi anaweza kupunguza vifo kwa asilimia 67.

Katika hilo, Dk Temu ameishukuru kampuni ya MCL inayozalisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen, Mwanaspoti na mitandao yake ya kijamii ikiwamo MCL Digital kwa kushirikiana na Amref kwa kuwasomesha ngazi ya vyeti wakunga 383.

Chanzo: mwananchi.co.tz