Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Ndugulile asikitishwa huduma za hospitali Zakhiem

47355 Ndugulile+pic

Tue, 19 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile ameonyeshwa kutoridhishwa na utendaji wa Hospitali ya Mbagala Zakhiem kutokana na dosari mbalimbali.

Dk Ndugulile amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo leo Jumatatu Machi 18, 2019 na kutoa maelekezo kadhaa kwa uongozi baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wagonjwa.

Miongoni mwa malalamiko ambayo Dk Ndugulile amepewa ni kukosekana kwa dawa, uchache wa wataalam hali inayosababisha msongamano pamoja na wahudumu kutoa kauli mbaya kwa wagonjwa.

Alipofika kwenye hospitali hiyo naibu waziri huyo ameshuhudia idadi kubwa ya watu wakingoja huduma huku ikionekana watoa huduma wamezidiwa.

Moja kwa moja Dk Ndugulile alianza kuwahoji wananchi kuhusu changamoto walizonazo na wengi walilalamikia kungoja huduma kwa muda mrefu.

“Nipo hapa tangu saa 11 asubuhi mtoto wangu anaumwa hadi sasa (ilikuwa saa 8 mchana) sijamuona daktari, hali hii inakatisha tamaa yaani,” amelalama Mariam Semi

Baada ya kusikiliza wananchi Dk Ndugulile alikwenda maabara ambako alikuta mashine mbili za kufanyia vipimo hazifanyi kazi kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Alipoulizwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dk Gwamaka Mwabulambo amesema hana taarifa kuhusu kuharibika kwa mashine hizo.

Jibu hilo limemfanya Dk Ndugulile kutoa maagizo kwa watendaji wote waliopewa dhamana ya kusimamia vituo vya afya kufuatilia utendaji wake.

“Kwa kweli hali ya Mbagala inasikitisha mashine zinaharibika DMO hajui, hakuna rekodi za vipimo maabara kwenye upande wa mapato ndio kabisa kuna udhaifu mkubwa,” amesema naibu waziri huyo.

“Sasa wito kwa wasimamizi wa hivi vituo na hospitali mfanye kazi yenu kwa uaminifu, mvitembelee kujua changamoto, lengo la Serikali ni kufikisha huduma za afya kwa wananchi kwa ukaribu,” amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz