Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Ndugulile aonya wanaokwamisha uwekezaji sekta ya afya

Wed, 3 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile ameonya watumishi wa Serikali wanaowawekea vikwazo wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika sekta ya afya nchini.

Amesema mbali na jitihada zinazofanywa na Serikali kuboresha sekta ya afya, bado ushiriki wa sekta binafsi katika sekta hiyo si mkubwa.

Dk Ndugulile amesema hayo leo Jumanne Oktoba 2 2018, wakati wa ufunguzi wa jukwaa lililowakutanisha wadau wa sekta binafsi kujadili masuala ya afya.

"Watumishi muache urasimu wa kuweka vikwazo kwa wawekezaji, siyo mtu anakuja mnaanza kumueleza mambo magumu mwisho wa siku anashindwa kuwekeza," amesema.

Lengo la jukwaa hilo la wadau wa sekta binafsi ni kuiboresha sekta hiyo muhimu ya afya.

Dk Ndugulile ameongeza kuwa kama Serikali haina haja ya kuingia gharama kununua vifaa mbalimbali vya tiba wakati sekta binafsi zina uwezo wa kuwekeza cha msingi wajengewe mazingira.

"Sisi hatuna haja ya kununua kifaa kimoja kimoja hawa wangeweza kununua vyote kwa pamoja na kuvisimamia," ameongeza.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz