Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Ndugulile: Sheria za makosa ya jinai zinajitosheleza

50652 Pic+ndugulile

Fri, 5 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali imesema licha ya sheria za makosa ya jinai kujitosheleza, bado kuna ugumu wa kuwatia hatiani wahalifu kutokana na kukosekana kwa ushahidi.

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa April 5, 2019 bungeni na Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustin Ndugulile ambaye ametaja changamoto inayokwamisha watuhumiwa kutiwa hatiani kutokana na matukio mengi kufanywa na watu walio ndani ya familia.

Alikuwa anajibu swali la msingi la mbunge wa Viti Maalumu, Zainab Bakar ambaye amehoji ni lini Serikali itapeleka muswada bungeni ili kutungwa kwa sheria kali ya ukatili, ubakaji na unajisi kwa watoto wa kiume.

Naibu Waziri amesema sheria zilizopo kwa sasa zinajitosheleza katika kuwashughulikia watu wanaokutwa na hatia ya makosa hayo

"Sheria ya makosa ya jinai imeelekeza adhabu kali kwa atakayebainika kutenda makosa hayo ikiwemo kifungo cha miaka 30 gerezani," amesema Ndugulile.

Amesema Serikali inajitahidi kuweka mikakati ya kusaidia kupunguza au kumaliza kabisa tatizo hili lakini akasema ushirikiano zaidi unahitajika.



Chanzo: mwananchi.co.tz