Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk. Mollel: Tutamshugulikia Askofu Gwajima

Screenshot 20210816 231118.png?fit=720%2C488&ssl=1 Dk. Mollel: Tutamshugulikia Askofu Gwajima

Tue, 17 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Siha, Mhe. Dkt. Godwin Mollel amemtaka Mbunge wa Kawe na Askofu wa Kanisa la ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kujitafakari juu ya madhara yatakayo wakuta wananchi kutokana na upotoshaji anaoendelea kuufanya na kuongeza kuwa hawezi kupingana na Serikali na hana uthibitisho wa kisayansi.

“Gwajima amevuka mipaka, anapotosha Taifa, hawezi kupingana na serikali na hana uthibitisho wa kisayansi, anasema mtu akichanjwa kuna vitu vinaingizwa mwilini ili mtu afe baada ya miaka miwili ama kumi, tutamuita athibitishe hili, akishindwa tutamshughulikia.

“Nimekuja kumuonya nikiwa kama mwana sayansi, ili ajue kwamba ametukanyaga sehemu, Gwajima anajua ukweli lakini ameamua kucheza ligi, tunamuonya tunataka awe na uthibitisho wa Kisayansi kwa kile anachosema kuhusu Chanjo ya Corona.

“Tumetumia nguvu nyingi sana kumuelemisha (Askofu Gwajima), tunataka tuthibitishiane kwamba sisi na yeye nani anataka kuiangamiza nchi, tujue nani anataka kuilinda nchi,” amesema Mollel.

Chanzo: globalpublishers.co.tz