Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk.Mollel: Msamaha wa matibabu ni kwa watu wasio na uwezo

WhatsApp Image 2022 06 09 At 1.37.51 PM.jpeg Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel

Fri, 10 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza kuwa na gharama kubwa na kuhitaji tiba wakati wote, Serikali imekuwa ikitoa masamaha wa matibabu kwa wagonjwa wanaougua magonjwa yasiyoambukiza ambao wamethibitishwa kuwa hawana uwezo wa kugharamia matibabu yao kwa maujibu bwa sera ya afya

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Chaani, Juma Usonge Hamad aliyehoji serikali ina mpango gani wa kutoa matibabu bure kwa maradhi yasiyoambukiza kama kisukari, presha na shinikizo la damu.

Hata hivyo Dk. Mollel amesema kuwa serikali ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa Muswada wa Bima ya Afya kwa wote ambao utawezesha wananchi wote kupata huduma za afya katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini.

Akijibu Swali la nyongeza lilioulizwa na Usonge aliyehoji usumbufu wanaopata wazee pindi wanapoenda hospitalini kupata huduma za matibabu, Dk. Mollel ameendelea kuwasisitiza wataalam kufuata maagizo yanayotolewa na viongozi ikiwemo kuhakikisha Wazee wanapata matibabu bure katika vituo vya kutolea huduma za afya.

“Nitumie fursa hii kutoa agizo kwa Waganga wote wa Mikoa na Wilaya, suala la matibabu kwa wazee ni bure na wanatakiwa kuwa na dirisha lao la kupata huduma, hatutegemei kusikia tena malalamiko ya wazee wanapitia mlolongo mrefu wa kupata huduma za matibabu” amesisitiza Dk. Mollel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live