Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk. Mollel: Asilimia Chache Wana Corona

MOLLEL?fit=588%2C344&ssl=1 Dk. Mollel: Asilimia Chache Wana Corona

Sun, 11 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel amesema asilimia kubwa ya wagonjwa waliofikishwa katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru wakihofiwa kuambukizwa corona hawana tatizo hilo bali wanasumbuliwa na magonjwa mengine ya mfumo wa hewa.

Dk. Mollel ameyasema hayo baada ya kutembelea hospitali hiyo kwa lengo la kujionea hali ambapo amesema kati ya wagonjwa 44 waliokuwa na matatizo ya kupumua ni wanne tu wamethibitika kuwa corona na wengine wana matatizo mengine yenye dalili zinazofanana na corona.

Aidha Dk. Mollell amewataka watendaji wa sekta ya afya na wananchi kwa ujumla kuendelea kuchukua tahadhari zote za kukabiliana na janga la corona kwani tatizo lipo.

Share this:TweetWhatsApp Related

Chanzo: globalpublishers.co.tz