Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Kigwangalla ahamishiwa Dar

10133 Maliasili+pic TanzaniaWeb

Sat, 4 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla ameondolewa katika hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center na kuhamishiwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Dk Kigwangalla amepata ajali leo Jumamosi Agosti 4, 2018 eneo la Magugu mkoani Manyara na kupata majeraha sehemu mbalimbali mwilini.

Katika ajali hiyo ofisa habari wa wizara hiyo, Hamza Temba amefariki dunia.

Soma Zaidi:

Kigwangalla apata ajali, kuhamishiwa hospitali kwa helkopta

Akizungumza na MCL Digital Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema licha ya waziri huyo kuendelea vizuri, anahitaji matibabu zaidi.

Amesema ndege itakayomchukua waziri huyo ipo Arusha na kwamba ataambatana na watu kadhaa.

Kuhusu mazishi ya Temba, amesema  yatafanyika kesho saa saba mchana nyumbani kwao  Masama wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Dk Kigwangalla aliondolewa katika hospitali hiyo akiwa pamoja na Milanzi, mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki.

Awali,  waziri huyo alipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Magugu na kuhamishiwa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center kwa helkopta.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz