Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Gwajima: ukatili unapelekea ugonjwa wa akili

Cd0489bd7be65b726388cb42003dd836 Dk Gwajima: ukatili unapelekea ugonjwa wa akili

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Dorothy Gwajima ametaja vinasaba, ukatili, na mtazamo hasi juu ya changamoto za maisha kuwa sababu zinazopelekea ugonjwa wa afya ya akili.

Amezitaja sababu hizo leo akiwa bungeni Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa viti maalumu CCM, Lucy Mayenga lililolenga kujua iwapo serikali ipo tayari kupunguza muda wa kuthibitisha wagonjwa wa akili walioko kwenye magereza na mahabusu mbalimbali nchini.

Akifafanua sababu za kibaiolojia, amesema mtu anaweza kuwa anaishi na vinasaba hivyo lakini asifikie hatua ya kupata ugonjwa huo. Pia amesema mazingira ya jamii anayoishi au mazingira yake binafsi yanaweza kumuandaa kupata au kutokupata ugonjwa huo.

Ametolea mfano wa matumizi ya vilevi kupita kiasi kwa mtu mwenye vinasaba, kama mazingira yanayoweza kuchochea kupata ugonjwa huo.

Chanzo: habarileo.co.tz