Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Gwajima aagiza Mganga Mkuu Chunya asimamishwe

1d4b3b3018b3b07cf64c3d2f862769d9 Dk Gwajima aagiza Mganga Mkuu Chunya asimamishwe

Mon, 8 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima, ameagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Chunya, Dk Felista Kisandu, asimamishwe kazi.

Waziri Gwajima jana aliagiza Baraza la Madaktari lifanye uchunguzi na apate taarifa ndani ya siku 10 juu ya ukiukaji wa taratibu za kutangaza magonjwa ya mlipuko kulikofanywa na Dk Kisandu.

Aidha hakuchukua hatua kujiridhisha kuhusu taarifa za kuwepo mlipuko wa ugonjwa usiofahamika kwenye Kata ya Ifumbo katika Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, kabla hajachakua hatua zinaozstahili kuarifu mamlaka.

Taarifa ya Dk Gwajima kwa umma jana ilieleza kuwa, hakuna mlipuko wa ugonjwa wowote uliothibitishwa na pia hakuna janga lolote la kiafya kama ilivyoripotiwa juzi kwenye vyombo vya habari.

Alisema kwenye taarifa hiyo kuwa, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila akiongoza timu ya wataalamu jana alikwenda kufuatilia suala hilo na alifanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Ifumbo ili kufahamu uhalisia wa jambo hilo.

Alisema timu ya wataalamu imefanya mahojiano na wananchi na kubaini kuwa, hakuna siku yoyote au mwezi wowote waliwahi kufariki dunia watu 15 kwa mara moja kwa wagonjwa wanaodaiwa kuwa na dalili za kutapika damu kama alivyoripoti Diwani wa Kata ya Ifumbo.

Alieleza kuwa Dk Kisandu hakuchukua hatua kujiridhisha kwa utaratibu wa miongozo ya kitaalamu na badala yake aliungana na Diwani kwenye ajenda hiyo hivyo alikiuka mwongozo wa utoaji taarifa za milipuko kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya Afya ya Jamii ya Mwaka 2009.

“Kwa kuwa chombo cha habari cha ITV nacho hakikuchukua hatua stahiki ya kujiridhisha kuhusu habari hiyo, wizara itachukua hatua za kupeleka malalamiko au mashitaka kwenye Wizara ya Mawasiliano katika vyombo husika vinavyohusika na maadili ya utoaji habari”ilieleza taarifa ya Dk Gwajima.

Chanzo: habarileo.co.tz