Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Gwajima, Mkurugenzi Switzerland kushirikiana kutoa huduma za afya

08fadc5f77e0b5f4f76f9311e6640f38 Dk Gwajima, Mkurugenzi Switzerland kushirikiana kutoa huduma za afya

Fri, 26 Nov 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Waziri wa Afa, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima na Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo na Ushirikiano wa Nchi ya Switzerland, Patricia Danzi wamekubaliana kushirikiana kuboresha huduma za afya nchini.

Dk Gwajima amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea kuboresha huduma za afya, na sasa ipo mbioni kupitisha sheria ya Bima ya Afya kwa wote itayomruhusu kila mwananchi kuwa na bima ili kupata huduma za matibabu.

Amesema kuwa Uswisi inatekeleza mradi mkubwa wa Mfuko wa Bima ya Afya ulioboreshwa ‘CHIF’ kwa maendeleo ya jamii unaogharimu Sh bilioni 24.3 utakao tekelezwa katika kilindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2019 hadi mwaka 2023.

Amesema Tanzania inaendelea kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria kupitia afua mbalimbali ikiwemo utoaji elimu kwa wananchi juu ya njia bora za kujikinga ugonjwa huo.

Dk Gwajima amesema Uswisi imeendelea kusaidia Tanzania Katika masuala ya utafiti wa magonjwa ambapo bajeti ya mwaka 2019 hadi 2024 zimetengwa fedha Sh bilioni 4.8 ambapo Tanzania imeendelea kuboresha huduma kwa kujenga vituo vya afya Zahanati na Hospitali za Rufaa .

Amesisitiza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuwakomboa wanawake kiuchumi kwa usawa wa kijinsia ambapo serikali imeandaa mpango kazi wa kuendeleza wanawake ili kuunda juhudi za serikali ya awamu ya sita.

Aidha, Dk Gwajima amesema kuwa, Tanzania inaendelea na mapambano dhidi ya UVIKO-19 kupitia afua ya Elimu kwa wananchi juu ya njia bora za kujikinga na maradhi na utoaji wa Chanjo ya UVIKO-19, huku akieleza tayari Tanzania imepokea Chanjo tofauti ikiwemo Jenseen, Sinopharm na Pfizer.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo na Ushirikiano ya Uswisi Patricia Danzi amesema Serikali ya Uswisi imekuwa mdau mzuri wa mapambano dhidi ya UVIKO-19 kwa kuchangia zaidi ya Dozi 4,000,000 kupitia Shirikisho la Kimataifa la Taasisi zinazoratibu upatikanaji na usambazaji wa chanjo ya uviko 19 ( COVAX Facility ) likijusisha nchi mbalimbali Dunia.

Viongozi hao wamekutana leo, katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma na kikao hicho kimehudhuriwa na baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Afya na Shirikishi la Maendeleo na Ushirikiano Uswisi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz