Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Gwajima: Bei elekezi taulo za kike yaja  

2d21325a7f4a7d439a9c78044d1569ea.jpeg Dk Gwajima: Bei elekezi taulo za kike yaja  

Tue, 25 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI iko mbioni kuja na mkakati madhubuti ya kusimamia kwa karibu utaratibu wa bei elekezi ya taulo za kike bila kuathiri ubora na wasichana wengi waweze kumudu.

Haya yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima katika maadhimisho ya Hedhi Salama ambayo kilele chake kitafanyika Ijumaa ya Mei 28 mwaka huu.

Amesema utafiti wa mwaka 2019 uliofanya na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) umebainikuwa asilimia 60 ya wasichana walionekana kutomudu gharama za taulo za kike.

Aidha, Dk Gwajima amesema kutokana na ongezeko la mahitaji ya matumizi ya taulo za kike ni vyema kwa watengenezaji, wauzaji na wasambazaji wa vifaa au taulo za kike, kuuza kwa bei nafuu ili kumuwezesha kila mwanamke au msichana kupata bidhaa hizi kwa urahisi huku wakizingatia ubora.

" Tutaratibu ajenda ya bei elekezi ya vifaa hivi bila kuathiri ubora. Hitaji hili la kuangalia bei za bidhaa hizi ni muhimu hasa tukizingatia kwamba kwenye utafiti wa NIMR unaonesha asilimia 60 ya wasichana walionekana kutomudu gharama za taulo za kike."

Chanzo: www.habarileo.co.tz