Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawa zaidi za asili zagundulika kutibu matatizo ya kupumua

B3aa5bff6b88d2efc0e95a1a4b82fe18 Dawa zaidi za asili zagundulika kutibu matatizo ya kupumua

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WATANZANIA wanaokumbwa na maradhi ya kushindwa kupumua vizuri na kubanwa mbavu wameshauriwa wasipate taharuki kwani kuna dawa ya asili inayotibu ugonjwa huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mtaalamu wa Tiba Asili, Baraka Beneza alisema dawa ya Mwalaka inayotengenezwa na Kampuni ya Altenative International Medicine imepata kibali cha Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto baada ya kuonekana kufikia viwango.

Alisema dawa hiyo inapatikana kirahisi na kuna ushuhuda wa watu wengi ambao wameshaitumia na kupata matokeo chanya baada ya kupata matatizo ya kupumua, kukohoa na kubanwa mbavu.

“Hii dawa inapatikana kirahisi Magomeni jengo la Butiama ilipo Benki ya DTB ni kinga na tiba, hivyo nawashauri watu wakiona dalili za kubanwa mbavu na kushindwa kupumua vizuri watumie dawa hii muda mfupi sana watakuwa wameshapata suluhisho,” alisema

Alisema dawa hiyo inatengenezwa kitaalamu na Alternative International Medicine kwa kushirikiana na kampuni ya MICO . Abdalah Chondoma ambaye aliwahi kuugua maradhi ya kushindwa kupumua, kubanwa mbavu na kukohoa sana alitoa ushuhuda kuwa baada ya kunywa dawa hiyo ya Mwalaka hivi sasa maisha yake yanaendelea kama kawaida.

Alisema alipata ugonjwa huo wakati akisafiri na basi kwenda msibani na wenzake lakini alipopatiwa dozi ya Mwalaka hali yake imetengemaa na anaendelea na kazi zake.

“Iliponishika nilikuwa nabanwa na mbavu, napumua kwa shida sana lakini dawa hii imenisaidia sana kwasababu ndani ya muda mfupi sana kifua changu kilifunguka na nikawa napumua vizuri na maumivu yaliisha,” alisema

Alisema watanzania wanapaswa kuchangamkia dawa hiyo kwani imewasaidia wananchi wengi waliokuwa na changamoto ya kupumua ambao wametoa ushuhuda wa walivonufaika.

“Dawa hii imesajiliwa rasmi na wizara husika kwa namba TZ 17TM 0035 kwa hiyo serikali inatambua kwamba ni dawa nzuri inayotibu kwa uhakika,” alisema Joyce Mwamtanga ambaye ni mjasiriamali wa vipuri, Kariakoo alisema wiki tatu zilizopita alibanwa mbavu na kushindwa kupumua lakini alipotumia dawa ya Mwalaka alipata nafuu ndani ya muda mfupi.

“Kwa kweli tuthamini bidhaa zetu zinazozalishwa hapa nchini kwasababu hii dawa ya miti ya asili imenisaidia sana inanguvu kwasababu baada ya kuitumia haikupita nusu saa nikajiona wa kawaida kabisa,” alisema Joyce.

Chanzo: www.habarileo.co.tz